.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 14 Oktoba 2015

ZEC YAENDESHA SEMINA KWA ASASI ZA KIRAIA KISIWANI PEMBA JUU YA UCHAGUZI MKUU WA 2015

DSC03711Kamishina wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Mh. Ayoub Bakar Hamadi akifungua semina maalum kwa asasi za kiraia kisiwani Pemba kuhusu Uchaguzi Mkuu 2015 ambayo ilifanyika tarehe 13/10/2015 ukumbi wa Hoteli ya Hifadhi Chake chake Pemba.DSC03703
Afisa Mdhamini, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Ndg. Ali Moh’d Dadi akitoa maeleo Mafupi kuhusu Semina za asasi za Kiraia iliyofanyika Hoteli ya Hifadhi Chake Chake Pemba Tarehe 13/10/2015.
DSC03717Afisa Habari na Uhusiano Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar BI, Salha Moh’d Ali akiwasilisha mada kuhusu mikakati ya Tume iliyofanywa juu ya utoaji wa Elimu ya Wapia Kura kwa Uchaguzi Mkuu 2015. aliwasilisha mikakati hiyo katika semina ya asasi za kiraia Pemba iliyoendeshwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanziba Tarehe13/10/2015 Ukumbi wa Hoteli ya Hifadhi Chake Chake Pemba.
DSC03722Mratibu wa Jumuiya ya Maendeleo Chokocho Bw. Shaali Makame Pandu akichangia hoja katika majadiliano yaliyofanywa na asasi za kiraia wakati wa semina iliendeshwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Hotel ya Hifadhi tarehe 13/10/2015. Semina hiyo ilikuwa na lengo kutoa elimu kwa asasi za kiraia juu ya Uchaguzi Mkuu 2015 na kuibua changamoto mbali mbali za elimu ya wapiga kura.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni