Majaji kwa upande wa Ubunifu wa Mavazi na Picha wakiwa kazini
Kutoka kushoto ni Iddy John , Sameer Kermalli na Angela Kilusungu ambao walikuwa majaji upande wa Picha, wanaofuata ni Comfort, Martin kadinda na Zamda waliokuwa majaji upande wa mavazi.
Kutoka kushoto ni Iddy John kutoka Wiki Love na Sameer Kermalli wakitazama kwa makini mmoja ya kazi za Mshiriki Ambaye (hayupo Pichani) Mmoja wa washiriki upande wa Ubunifu wa Mavazi(aliyesimama kulia) akielezea kazi zake kwa majaji
Majaji kwa upande wa ubunifu wa mavazi wakitoa alama zao kwa mmoja ya washiriki ambaye (hayupo pichani)
Baadhi ya Washiriki wa Ubunifu wa mavazi wakionesha kazi zao wakati wa kuwatafuta washiriki 5 Bora
Baadhi ya Washiriki kwa upande wa Picha wakiwa wanaonesha kazi zao kwa Majaji ambao (hawapo Pichani) wakati wa kuwatafuta tano(5) bora.
Hatimaye Shindano la Bongo Style linalo andaliwa na Faru Arts and Sports Development Organization(FASDO) lililo anzishwa mwaka huu na ambalo litakuwa likifanyika kila mwaka lililowahusisha vijana wenye umri kati ya Miaka 18-25 wakiwemo wapiga picha na wabunifu wa mavazi 20 waliokuwa wamechaguliwa kuingia Nusu Fainali baada ya kujiandikisha kushiriki shindano hili kwa kupitia tovuti ya FASDO www.fasdo.org na kuchaguliwa toka kwa washiriki 300 waliojiandikisha limefikia hatua ya Fainali.
Katika hatua hiyo ambayo ilikuwa ngumu kutokana na kuwa kila mshiriki alikuwa na radha yake tofauti ya ubunifu katika kazi yake kwa vipengele vyote viwili picha na ubunifu wa mavazi, ambapo wamepatikana washiriki 10 ambao ndio wanaendelea na Shindano hili mpaka siku ya Fainali tarehe 28.11.2015, zitakazofanyika katika ukumbi wa ndani wa Alliance Francaise Jijini Dar es salaam.
Vijana hao walioshinda hatua ya Fainali kwa upande wa Picha ni pamoja na Rasheed H Rasheed Hamis (24) Dar es salaam, Daniel Msirikale (24) Dar es salaam, Hassan Mohamed (24) Dar es salaam, Aneth Ngowano (21) Dar es salaam na Trevor Gaudence (23) Dar es salaam. Kwa upande wa ubunifu wa mavazi waliopita ni pamoja na Jocktan Makeke(25) Iringa, Winfrida Touwa (21) Mwanza, Anna Ben Paul (23) Dar es salaam, Lilian Ndashau (24) Dar es salaam na Shahbaaz Yusuph (19) Dar es salaam.
Akieleza juu ya shindano hili baada ya kupatikana majina ya watakao ingia fainali, Mratibu wa FASDO Tanzania Joyce Msigwa alisema washindi wawili kati ya kipengele cha picha na ubunifu wa mavazi watapata Tsh 1,000,000 kila mmoja na nafasi ya kwenda Uberigiji kwa wiki mbili. Aliongeza kuwa washiriki wote wa nusu fainali watapata nafasi ya kutangaziwa kazi zao bure kwa muda wa mwaka mmoja na kushiriki katika masomo/mafunzo mbalimbali pindi yatakapo tokea, mwisho alisema shindano hili litakuwa linafanyika kila mwaka.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni