Askari magereza muandamizi katika
gereza la Naivasha GK nchini Kenya amekamatwa akijaribu kuingiza
gerezani misokoto 1,800 na simu 18.
Afisa huyo mwenye cheo cha Inspekta
Mkuu alinaswa akiwa ameficha misokoto ya bangi 1,772 kwenye matairi
ili kuwapelekea wafungwa zaidi ya 3,000.
Kwa muibu wa chanzo cha habari mkuu
wa gereza alifahamishwa juu ya biashara hiyo na ndipo alipoendesha
operesheni hiyo iliyofanikisha kunasa misokoto hiyo na simu 18.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni