Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Yamungu Kayandabila akizungumza na wadau wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia katika mkutano maalum wa siku ya Sayansi Duniani. Kushoto kwake ni Afisa utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO- Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam Novemba 10. 2015. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
Afisa Utawala na Fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha ambaye alimwakilisha Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa UNESCO- Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akisoma ujumbe maalum wa siku ya Sayansi Duniani wakati wa mkutano huo wa wadau wa Sayansi.
Profesa John Kondoro Mkuu wa Chuo cha Teknolojia cha jijini Dar es Salaam – (DIT) akitoa mada katika mkutano huo wa wadau wa Sayansi wakati wa maadhimisho ya siku ya Sayansi.
Afisa kutoka UNESCO NAT.COM, Bw. Joel Samuel akitoa mada katika mkutano huo wa wadau siku ya Sayansi Duniani.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye, akifafanua jambo wakati wa mjadala huo juu ya maendeleo ya Sayansi na Teknolojia nchini katika mkutano uliowakutanisha wadau wa Sayansi katika maadhimisho ya Siku ya Sayansi Duniani.
Wadau wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa siku ya Sayansi Duniani.
Na Andrew Chale, Modewjiblog
[DAR
ES SALAAM-TANZANIA] Tanzania kupitia wadau wa Sayansi nchini
imedhamilia kupiga hatua zaidi katika kufikia malengo ya Agenda 2030 kwa
kuchangamkia fursa za maendeleo katika Sayansi.
Hayo yameelezwa
jijini hapa wakati wa wadau wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
walipokutana katika majadala wa Siku ya Sayansi Duniani kwa ajili ya
Amani na Maendeleo (World Science Day for Peace and Development).
Akisoma
neno, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
Dkt. Yamungu Kayandabila amelipongeza Shirika la Kimataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO), katika kukuza Sayansi nchini.
Dkt.
Yamungu ameelezea kuwa, nchi yoyote ile ilikuendelea, inategemea
Sayansi hivyo kwa Tanzania ni wakati wa kuchangamkia fursa ili kufikia
malengo na Agenda 2030.
“Tanzania tuna fursa nyingi na za
kutosha. Tuna Nyuklia na hii ni uchumi tosha tutakapofanyia kazi kwa
malengo tutafika mbali kwani inahitaji Sayansi ya kina.
Navipongeza
vyuo mbalimbali vilivyopo nchini ikiwemo DIT, Nelson Mandela cha
Arusha, Chuo cha Sayansi Mbeya na vingine vingi” ameeleza Dk. Yamungu.
Aidha,
Dkt. Yamungu ametaka Sayansi kuendana na suala la ulinzi wa chakula na
miundombinu mingine ikiwemo suala la maji huku akihimiza wanafunzi
kuyapenda na kuyasoma masomo ya Sayansi na suala la umuhimu wa Sayansi
na namna inavyoweza kuathiri maisha ya watu kila siku.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Sayansi na Teknolojia Prof. Evelyn Mbede
amepongeza wadau wa Sayansi na Teknolojia kwa kujimuika katika
maadhimisho ya siku hiyo ya Sayansi Duniani ambapo ameelezea kuwa Wizara
yake milango ipo wazi kwa wadau wote katika kuhakikisha wanapiga hatua
katika kukuza na kuendeleza Sayansi hapa nchini.
Kwa upande wake,
Afisa Utawala na Fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha ambaye alimwakilisha
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO- Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues
alipongeza juhudi za Serikali ya Tanzania katika kutilia mkazo suala la
Sayansi na Teknolojia na kufanya suala hilo kuwa mtambuka kwa maendeleo
ya vizazi vya sasa na baadae.
Akisoma ujumbe maalum kutoka
UNESCO, Bw. Bokosha alieleza kuwa kupitia Sayansi na Teknolojia na
ubunifu, maendeleo ya Taifa endelevu, uimarishaji wa mazingira ikiwa ni
pamoja na kuongezeka kwa maandalizi kwa ajili ya kukabiliana na
Mabadiliko ya Tabianchi na madhara yake hivyo Sayansi inahitajika kwa
kiwango kikubwa juu ya hilo.
Aidha, ameeleza kuwa, UNESCO imekuwa
mstari wa mbele katika kuanzishwa kwa moduli za elimu ya Mazingira
katika shule za Sekondari.
Akinukuu ujumbe maalum kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi Irina Bokova katika ujumbe alieleza:
“Hii
ni siku ya Sayansi Duniani kwa amani na Maendeleo na imekuja miezi
miwili baada ya makubaliano ya Agenda 2030 ya maendeleo endelevu.
Hivyo
Serikali zote zitambue nguvu ya Sayansi ya kutoa majibu muhimu kwa
usimamizi mzuri wa maji kwa ajili ya hifadhi na matumizi endelevu ya
bahari, ulinzi wa mazingira na viumbe hai, ilikukabiliana na mabadiliko
ya tabianchi na majanga na kuendeleza uvumbuzi na kuondokana na
umasikini na kupunguza tofauti” alieleza katika nukuu hiyo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni