Mwanamuziki anayekuja kwa kasi katika tasnia
ya muziki Bongo, Fredrick Kalala ama jina la usanii akijulikana zaidi,
Fred Swagg ameachia wimbo mpya mtandaoni ‘NIMEWAKA’ au
‘Nimelewa’.
Akizungumza na Modewjiblog kwa njia ya simu
kutoka jijini Mwanza, Fred Swagg mkali wa vibao vya Maandishi
alichowashirikisha Younf Killer na Kad Go. Ameeleza kuwa katika wimbo
wake huo mpya wa Nimewaka, upo katika mahadhi ya rap, ni maalum kwa
watu wa rika zote hasa sehemu za starehe ikiwemo
Club.
“Wimbo huu mpya wa Nimewaka ni wa ku-Party’
ndani yake kuna komediani ikielezea watu wanavyotumia pesa na kulewa
pombe za aina mbalimbali.. hivyo fans wakae mkao wa kula kuanzia sasa
itakuwa mtandaoni ikiwemo mkito.com “ ameleza Fred Swagg.
Fred Swagg anabainisha video ya wimbo huo
zinatarajia kuanza muda wowote kuanzia mwezi ujao huku kwa sasa
akiendelea na promo za nyimbo zake zingine zinazofanya vyema kwenye
vituo vya radio mbalimbali za ndani na nje wimbo wa ‘Kikomo’
aliomshirikisha Msanii, Da Prince na wimbo wa Maandishi
aliowashirikisha Young Killer na
Kad-

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni