Timu ya Chelsea inahofiwa Eden
Hazard ataitwa kuwa shahidi wa daktari wao Eva Carneiro katika shauri
dhidi ya klabu hiyo la kuacha kazi kutokana na kukerwa na muajiri
wake mwaka jana.
Daktari huyo wa zamani wa Chelsea
ameacha jukumu lake hilo katika klabu hiyo baada ya kutupiana maneno
hadharani na Jose Mourinho baada ya Hazard kuumia dakika za mwisho
katika mchezo ulioishia kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Swansea City,
Agosti 8.
Ingawa Hazard anasita kujihusisha na
kesi hiyo, winga huyo wa Chelsea anaweza kulazimishwa na Mahakama ya
Baraza la Kazi inayosikiliza shauri hilo.
Dokta Eva akimtibu Hazard baada ya kuumia
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni