Baadhi ya waliokuwa washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula kwa nyakati tofauti wakionesha bidhaa zao

Kushoto ni mmoja wa washiriki waliohudhulia kongamano la mabadiliko ya Tabianchi akipokea zawadi ya tsh 100,000 aliyoshinda Steven Albert.
ASASI za Kiraia nchini zikiwemo Oxfam Tanzania, Forum CC na Norwegian Church Aid Actalliance zafanya kongamano la Kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa Chakula nchini.
Akizungumza Afisa Miradi Msaidizi wa Shirika la Forum CC,Jonathan Sawaya alisema asasi hizo zimeona ni vema kuwakilisha sauti za wakulima kwa serikali katika kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.
Alisema asilimia kubwa ya wakulima wengi hasa wanawake ambao karibia asilimia 70 wamekuwa wakiathirika na Mabadiliko hayo wakati wanapolima.
Sawaya alisema wananchi wanapaswa kuhifadhi mazingira na kutunza vyanzo mbalimbali vya maji ili kupunguza athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.
"Kwa kushirikiana na shirika la Oxfam pamoja na Norwegian Church Aid tumeamua kufanya kongamano hili ili kupaza sauti za wakulima na wafugaji katika suala zima la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na serikali kutilia mkazo katika kusimamia suala hili kwa kuongeza bajeti,"alisema Sawaya
Aidha alisema asilimia kubwa ya wanawake wameonyesha juhudi mbalimbali za kukabiliana na athari hizo kutokana na wao kujihusisha katika uzalishaji wa chakula.
"Tuwaunge mkono wazalishaji wa chakula wadogo,wafugaji pamoja na wavuvi katika suala hili kwa kuwaunganisha na masoko na kuwapa mikopo,"alisema
Aidha Kongamano hili limehusisha wadau mbalimbali wakiwemo watendaji wa serikalini,wakulima pamoja na wafugaji katika kuhakikisha mabadiliko ya tabia nchi yanatokomezwa.
"Kongamano hili ni sehemu ya maandalizi ya Mkuu wa 21 wa Mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi unaotarajia kufanyika Novemba 30 nchini Ufaransa,"alisema Sewaya
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni