.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 4 Novemba 2015

LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA, REAL MADRID YAIFUNGA PSG, BAO LA KICHWA LA ROONEY LAIBEBA MANCHESTER UNITED DHIDI YA CSKA MOSCOW NAO SEVILLA WAKIONA CHA MOTO NYUMBANI KWAO MBELE YA MANCHESTER CITY

Ligi ya mabingwa barani Ulaya imeendelea usiku wa kuamkia leo katika viwanja mbalimbali barani humo, na katika uwanja wa Santiago Bernabeu wenyeji Real Madrid wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wafaransa Paris St Germain ( PSG ). Bao pekee la Madrid lilifungwa na Nacho katika dakika ya 35
Mshambuliaji mahiri wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ( kulia ) akimpongeza Nacho baada ya kufunga bao pekee lililodumu hadi mchezo unamalizika.
Katika mchezo mwingine wa ligi ya mabingwa barani Ulaya uliochezwa usiku wa kuamkia leo katika uwanja wa Old Trafford, uliishuhudia Manchester United ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya CSKA Moscow waliosafiri kutoka Urusi. 

Katika mchezo huo, mshambuliaji Wayne Rooney ndiye aliyekuwa shujaa wa Manchester United baada ya kuifungia timu yake bao hilo muhimu kwa kichwa katika dakika ya 79 ya kipindi cha pili cha mchezo huo.
Kocha mkuu wa Manchester United, Mholanzi Van Gaal akiwashukuru mashabiki wao baada ya kumalizika kwa mchezo huo.
Wenyewe Manchester City wakicheza ugenini katika mchezo mwingine wa ligi ya mabingwa barani Ulaya waliibuka na ushindi mzuri wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji wao Sevilla. 

Mabao ya haraka haraka ya kipindi cha kwanza kupitia kwa Raheem Sterling aliyefunga bao la kwanza dakika ya 8 na Fernandinho akifunga la pili kunako dakika ya 11 yalionekana kuwachanganya wenyeji Sevilla waliolazimika kupambana na kupata bao katika dakika ya 25 likifungwa na Tremoulinas. 

Kuingia kwa bao hilo ni kama kulichochea hasira za Manchester City, kwani kabla ya kwenda mapumziko walijipatia bao la tatu lililofungwa na Bony dakika ya 36. Hadi mwisho wa mchezo huo, Sevilla 1 na Manchester City 3.







Hakuna maoni :

Chapisha Maoni