Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn (kulia) akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Bernard Membe alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kushiriki sherehe za uapisho za Rais Mteule, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Nyusi akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kushuhudia sherehe za uapisho wa Rais Mteule, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Zambia, Mhe. Edger Lungu akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kushuhudia sherehe za uapisho wa Rais Mteule, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni