.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 24 Novemba 2015

MAREKANI YATEKETEZA ZAIDI YA MALORI YA MAFUTA 238 YANAYOMILIKIWA IS NCHINI SYRIA

Mashambulizi ya anga ya Marekani yameteketeza zaidi ya malori ya mafuta 238 yanayomilikiwa na kundi ya Dola ya Kiislam (IS), kaskazini mashariki mwa Syria.

Imeelezwa kuwa rubani wa ndege ya kivita ya Marekani aliyakuta malori hayo yakiwa yameegeshwa katika maeneo ya kuzalisha mafuta karibu na al-Hasakah na Dayr Az Zawr.

Kabla ya kuyashambulia malori hayo mashambulizi ya kuwatahadharisha madereva wa malori hayo ambao ni raia wa kawaida yalifanywa ili wakimbie na kisha kuyashambulia malori hayo.

Kundi la wapiganaji wa Dola ya Kiislam linapata mapato makubwa ya fedha kutoka kwa maeneo ya visima vya kuzalisha mafuta waliyoyateka.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni