Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mh Amos Makalla akipewa maelezo wakati akikagua kituo cha kufua Umeme bwawa la Nyumba ya Mungu
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mh Amos Makalla akitoa maelekezo baada ya kukagua kituo cha kufua Umeme bwawa la Nyumba ya Mungu
Akiwa katika kituo cha kufua Umeme amekipongeza kituo kwa kufanya kazi Nzuri ya kuchangia Umeme megawatt 8 katika gridi ya Taifana hivyo amewataka kufanya kazi kwa bidii ili kukabiliana na changamoto za upungufu wa umeme kwani wakibweteka watasababisha upungufu wa hizo megawatt 8 katika gridi ya taifa
Aidha ameitaka serikali ya wilaya ya Mwanga kusimamia wavuvi hawavamii hifadhi ya Tanesco ili kutohatarisha uharibifu katika chanzo cha kufua Umeme
Katika mradi mkubwa wa Maji wa Same-Mwanga- Korogwe mkuu wa mkoa ameridhishwa na kazi aliyoianza mkandarasi na amehaidi atashirikiana na wizara ya Maji na Fedha kumlipa mkandarasi fedha ili aendelee na kazi
Ameeleza kuwa mradi wa Same- Mwanga anauelewa vizuri kwa kuwa alikuwa Naibu wa Maji na ziara hii ni ya pili . " mradi huu naufahamu vizuri unagharimu dola za kimarekani milioni 41 na mkataba wake ni miezi 31 Na inatarajiwa kukamilika Julai 2017 na utanufaisha Vijiji 17 mwanga, Vijiji 16 same na Vijiji 5 wilaya ya korogwe "
Amewataka wananchi kutoa ushirikiano na mkandarasi na ameelekeza ajira za kazi zenye kufanywa na watanzania wawajiri watanzania
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni