Mlipuko umelilenga basi lililokuwa
limebeba walinzi wa rais katika Jiji la Tunis nchini Tunisia na kuuwa
watu 12.
Kufuatia tukio hilo rais Beji Caid
Essebsi ametangaza siku 30 za hali ya hatari na kutangaza watu
kutotembea ovyo katika Jiji la Tunis.
Tunisia imekuwa ikikapiliwa na
mashambulizi ya kundi la Dola ya Kiislam (IS), likiwemo tukio la mtu
mwenye silaha kuwashambulia watu kwenye hoteli ya ufukweni ya Sousse
mwezi Juni na kuuwa watu 38.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni