.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 12 Novemba 2015

MTOTO WA MWAKA MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KISIMANI MBEYA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi.

                                                                                    Na EmanuelMadafa,Mbeya

Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi saba Promis Dank mkazi wa bwawani wilaya ya chunya alifariki dunia njiani akiwa anapelekwa hospitali baada ya kutumbukia kisimani.

Tukio hilo limetokea Novemba 112 majira ya saa 12 asubuhi huko kitongoji cha railway, kata ya bwawani, wilaya ya chunya, mkoa wa mbeya.

Inadaiwa kuwa, mtoto huyo baada ya kutumbukia kwenye kisima hicho ambacho kilikuwa wazi, aliokolewa akiwa hai lakini alifariki dunia akiwa njiani kuelekea hospitali teule ya mwambani kwa matibabu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed z. Msangi ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwa makini hasa kwa kuweka uangalizi wa kutosha kwa watoto wadogo ili kuepuka madhara yanayoweza kuepukika.

Aidha anatoa wito kwa jamii kufunika visima vilivyowazi, kufukia mashimo yenye maji kwani ni hatari kwa watoto wadogo hasa katika msimu huu wa mvua za vuli.   (JAMIIMOJABLOG MBEYA )

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni