Polisi nchini Ubelgiji wamewakamata
watu 16, katika msako wa kukamata magaidi hata hivyo mhusika wa
mashambulizi ya Paris, Salah Abdeslam, bado hajulikani alipo.
Polisi wamevamia maeneo 22 siku ya
jumapili katika Jiji la Brussels na Charleroi, mwendesha mashtaka wa
Ubelgiji, Eric van der Sypt, ameviambia vyombo vya habari.
Polisi walilifyatulia gari moja
risasi mbili katika operesheni hiyo eneo la Molenbeek, na kumjeruhi
mtuhumiwa mmoja ambaye baadae alikamatwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni