.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 2 Novemba 2015

SHULE YA MSINGI GREEN HILL YA JIJINI DAR ES SALAAM YAFANYA VIZURI KATIKA MTIHANI WA DARASA LA SABA.

New Picture (3)
                                                                                     Na:George Binagi-GB Pazzo 

Shule ya Msingi Green Hill iliyopo Ilala Mkoani Dar es salaam imekuwa miongoni mwa shule bora zilizofanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba, uliofanyika mwezi Septemba mwaka huu kote nchini.
 

Katika Matokeo yaliyotangazwa jana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini NECTA Dk.Charles Msonde, ufaulu wa Kitaifa mwaka huu umepanda kwa asilimia 10.85 kutoka asilimia 56.99 za mwaka jana, ambapo wanafunzi waliofaulu ni 518,034 kati ya 775,273 waliosahiliwa mwaka huu.
 

Kwa upande wa Matokeo ya Msingi Green Hill, Matokeo yanaonyesha kuwa shule hiyo imeshika nafasi ya saba kati ya shule 56 katikaWilaya ya Ilala, nafasi ya 39 kati ya shule 634 katika Mkoa wa Dar es Salaam na nafasi ya 324 kati ya shule 16,096 Kitaifa.
 

Wahitimu wote 93 wa shule hiyo wakiwemo wa kume ni 45 na wa kike 48 wamefaulu mtihani wao kwa madaraja yote ya ufaulu jambo lililofanya shule hiyo kupokea pongezi mbalimbali kutoka kwa wazazi na walezi wa wahitimu hao kwa njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni