UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umewaomba radhi wadau wa
soka pamoja na shirikisho la soka nchini (TFF) kwa vurugu zilizotokea kwenye mchezo wa baina yake na Mbeya City uliofanyika mwishoni mwa wiki uwanja wa CCM Mkwakwani.
Mchezo huo wa ligi kuu Vodacom ulimalizika kwa vurugu hadi kikosi cha kutuliza ghasia kilipoingilia kati na kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya mashabiki wa soka waliokuwepo katika uwanja wa Mkwakwani.
Vurugu hizo zilitokea kufuatia mwamuzi,Erick Enock kutoka Arusha kuamuru ipigwe penati kuelekea lango la Coastala union katika dakika za majeruhi na kuiwezesha Mbeya City kusawazisha bao hivyo hadi matokeo kuwa sare ya fungana bao 1-1.
Coastal Union iliomba radhi katika barua yake iliyoandikwa na kutiwa saini na Mwenyekiti wake,Dr Ahmed Twaha kwenda kwa Katibu mkuu wa TFF na nakala kwa Rais Jamal Malinzi,afisa mtendaji mkuu bodi ya ligi na katibu wa Chama cha soka mkoa wa Tanga (TRFA).
Aidha baada ya kutokea tukio hilo,Mwenyekiti huyo alisema alilazimika kuitisha kikao cha dharura cha kamati ya utendaji kujadili nini cha kufanya na hatua za kuchukua kwa wale watakaobainika kuhusika kwenye vurugu hizo.
Katika kikao hicho alisema kamati ya utendaji imelaani vurugu hizo na imeaziamia kuwachukulia hatua waliohusika“Tunaomba radhi kwa TFF na TRFA kwa matukio hayo yaliyofanywa oktoba
31,tunachukua ahadi klabu ya Coastal Union kufidia gharama za uharibifu utakaothibitika na kuwachukulia hatu waliohusika”ilieleza sehemu ya barua hiyo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni