Timu za taifa za Sweden na Ukraine
zimekua timu za mwisho kuzufu katika michuano ya Ulaya ya mwaka 2016
itakayofanyika nchini Ufaransa.
Sweden wakicheza ugenini walitoka
sare ya mabao 2-2 dhidi ya Denmark, na kufanikiwa kufuzu baada ya
kushinda mchezo wa kwanza kwa ushindi wa mabao 2-0.
Mshambulia Zlatan Ibrahimovic ndiye
aliyefunga mabao yote mawili ya Sweden huku yale ya Denmark,
yakifungwa na Yussuf Poulsen na Jannik Vestergaard.
Zlatan Ibrahimovic akiangalia mpira wa adhabu alioupiga ukielegea golini
Kipa wa Denmark akiambulia hewa wakati mpira uliopigwa na Zlatan ukitinga wavuni.
Ukraine nao wakatinga kwenye fainali
za Ulaya licha ya kwenda sare ya bao 1-1 na Slovenia, ambapo katika
mchezo wa kwanza Ukraine walishinda kwa mabao 2-1.
Timu 24 zilizofuzu kushiriki
michuano hiyo ya ulaya ni wenyeji Ufaransa, Albania, Austria,
Ubelgiji Croatia, jamhuri ya Czech, Uingereza, Ujerumani, Hungary,
Iceland, Italia, Ireland ya Kaskazini, Uholanzi, Ureno, Jumhuri ya
Ireland, Romania, Urusi, Slovakia, Hispania, Sweden, Switzerland,
Uturuki, Ukraine na Wales.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni