Uhusiano baina ya nchi ya Rwanda na
Burundi upo katika hali tete kufuatia serikali ya Burundi kuishutumu
Rwanda kwa kuwaunga mkono wapinzania wa serikali ya Pierre Nkurunziza
iliyomadarakani kwa muhula watatu.
Katika hotuba yake wakati wa utoaji
tuzo Jijini Kigali rais Paul Kagame wa Rwanda ameshutumu ongezeko la
ghasi katika nchi ya Burundi, wakati ikianza msako wa kuwadhibiti
watu wenye silaha.
Burundi imekuwa katika machafuko
tangu Aprili mwaka huu, ambapo rais Kagame amesema kuwa watu wamekuwa
wakiuliwa kila siku na miili yao kukutwa mitaani, huku viongozi
wakitumia muda wao kuuwa watu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni