.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 2 Novemba 2015

WAKAZI WA JIJI LA MWANZA WATAABIKA NA MAFURIKO KUTOKANA NA MVUA INAYOENDELEA KUNYESHA.

Miongoni mwa nyumba zilizopo Mtaa wa Kilimahewa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza ambazo huathirika na kero ya Maji kuingia ndani pindi mvua zinapoanza kunyesha.
 

Pichani ni mmoja wa wakazi wa Kilimahewa akitoa maji ndani ya nyumba yake kutokana na mvua iliyoanza kunyesha majira ya saa kumi na mbili alfajiri hii leo. Hadi tunaenda hewani (saa 10:30 asubuhi) Mvua hiyo inaendelea kumiminika mdogomdogo.  Picha na Loyce Nhaluke
 

Mbali na Kilimahewa, Pia wakazi wa Mabatini Jijini Mwanza hukumbwa na kero ya Mafuriko wakati wa Mafuriko na kwa miaka mingi juhudi za kuwahamisha zimekuwa zikigonga mwamba linapokuja suala la kuwatafutia makazi mapya.
 

Mara kadhaa mafuriko katika maeneo hayo yamekuwa yakisababisha athari mbalimbali ikiwemo vifo.
Maji hadi ndani, hakika ni hatari
Maji yakitolewa ndani
Kilimahewa Manispaa ya Ilemela
Binagi Media Group, Kwa Pamoja Tuijuze Jamii

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni