.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 30 Novemba 2015

WAKULIMA ZAIDI YA 300 WA MKOA WA MTWARA WAJIUNGA NA NSSF


SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeandikisha wakulima wa Korosho zaidi ya 300 mkoani mtwara kwenye kampeni ijulikanayo kama NSSF Kwanza ambayo ilifanyika mahususi ili kuwafikia watu ambao wako kwenye sekta isiyo rasmi.
 
Kampeni hiyo yenye malengo ya kufikia umma wa Watanzania ambao haujafikiwa na elimu ya Hifadhi ya jamii, Kuwaandikisha kujiunga na NSSF ili kuongeza wigo wa wanachama na pia Kupata mrejesho wa huduma zetu kutoka kwa wanachama wa mfuko.
 
Imemaliza mkoani Mtwara na itaendelea kwenye mikoa mingine.

NSSF inaendelea kuwasihi Watanzania waendelee kujiunga na NSSF.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni