Kutochukua hatua za haraka kwa
Jumuiya ya Kimataifa na kushindwa kwa uongozi kumeshutumiwa kwa
kusababisha mateso na vifo visivyo vya lazima vya mlipuko wa hivi
karibuni wa ugonjwa Ebola.
Jopo la wataalam likiongozwa na
Shule ya Magonjwa ya Tropika na Usafi ya London limetoa shutuma hizo
katika ripoti yake iliyotaka kufanyika mabadiliko yatakayoweza kuzuia
janga la ugonjwa huo kutokea katika siku za baadae.
Zaidi ya watu elfu 11 walikufa
katika mlipuko wa Ebola ulionza mwaka 2013 na kuathiri mno nchi za
Guinea, Liberia pamoja na Sierra Leone.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni