Watu milioni 11 wapo hatarini kwa
njaa, maradhi na uhaba wa maji mashariki na kusini mwa bara la
Afrika, kutokana na kuimarika kwa hali ya hewa ya El Nino, Shirika la
Umoja wa Mataifa limesema.
Shirika la hilo la Umoja wa Mataifa
la Kuwahudumia Watoto (Unicef) limesema hali hiyo imesababisha ukame
hatari kuwahi kutokea kwa zaidi ya miaka 30 nchini Ethiopia.
Shirika la Unicef limesema madhara
ya hali ya hewa ya El Nino yanaweza kuwa mabaya pia kwa Somalia huku
pia kukiwa na hofu ya kutokea mafuriko. El Nino husababishwa na hali
ya joto katika bahari ya Pacific.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni