Watu wapatao 10 wamekufa katika
tukio la shambulio la kujitoa mhanga kwenye hoteli katika Jiji Kuu la
Mogadishu nchini Somalia.
Polisi wamesema watu wenye silaha
walitumia gari lililojaa milipuko kuingia kwa nguvu katika eneo la
hoteli na baadae kuvamia jengo la hoteli hiyo.
Vikosi vya Umoja wa Afrika na vikosi
vya serikali vimesema vimefanikiwa kuwadhibiti wapiaganaji waliotwaa
hoteli hiyo baada ya mapigano makali. Hoteli hiyo ni maarufu kwa
kuwapo wabunge wa Somalia.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni