.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 27 Novemba 2015

ZIARA YA PAPA FRANCIS NCHINI KENYA

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis akiwasili katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya tayari kuendesha misa iliyohudhuriwa na maelfu ya waumini wa dini ya Kikristo licha ya kuwepo mvua. 

Katika misa hiyo Papa aliwataka vijana kujenga jamii moja ambayo ni imara, pia aliwaambia wakenya wasiogope jambo lolote kwa kuwa wao ni mali ya Mungu, na kuwataka wasimame pamoja katika imani huku pia Papa akionekana kukerwa na rushwa na utoaji mimba.
Maelfu ya wananchi wakiwa wamefurika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Nairobi wakisubiri kuanza kwa misa ambayo iliongozwa na Papa Francis. 

Ziara yake nchini Kenya inakamilika leo, na jioni anatarajiwa kuelekea nchini Uganda ikiwa ni katika nchi za Afrika zilizo katika ratiba yake ya kuzitembelea kabla hajakamilisha ziara yake barani Afrika kwa kutembelea Jamuhuri ya Afrika ya Kati.





Hakuna maoni :

Chapisha Maoni