Na mwandishi wetu.
Hospitali za Apollo zimefanikiwa kwa mara ya kwanza barani Asia kufanya
upandikizaji wa moyo na ini; hivyo kujiunga na timu ya hospitali chache
duniani zilizowahi kufanya upasuaji huo wa aina
yake.
Desemba 2015; Hospitali za Apollo
ambazo ni kinara barani Asia kwa ubora wa huduma za afya, kwa mara
nyingine zimeonyesha ubora wake wa uongozaji kupitia kituo cha
upandikizaji duniani kwa kufanikisha upasuaji wa upandikizaji kwa mpigo
wa ogani za moyo na ini kwa kijana mwenye umri wa miaka 30
anayetokea Tiruchengode,
Tamilnadu nchini India.
Tukio hilo linalotambulika kitaalam
kama CHLT ni mfumo mgumu wa upasuaji
na haujawahi fanyika popote barani Asia. Kama ilivyoitwa na chuo cha
Stanford kuwa ni “upasuaji wa kiufundi na kitaalam sana, ambao ni vyema
uachwe kwenye mikono ya madaktari bingwa wenye ujuzi”, ni hizo hatua za
CHLT pekee zimeweza kufanyika ulimwenguni
pekee.
Stori hii ya Ndg.
Ponnar, kijana mtulivu kutokea Tiruchengode, mji mdogo kutokea wilaya ya
Namakkal Tamilnadunchini India. Ponnar alikuwa ni mwanafunzi bora
aliyemaliza stashahada yake kwenye fani ya uhandisi na alikuwa na medali
ya dhahabu.
Katika umri wa miaka 22, kama kijana mwenye malengo makubwa
na matumaini ya kufikia ndoto zake, Ponnar alianza kuhisi kujaa maji
tumboni mwake, upungufu wa pumzi na kujikuta rangi ya ngozi yake kuanza
kuwa manjano.
Hii ilitambulika
kama kufeli kwa ini, iliyopelekea kufanyiwa kwa upandikizaji wa ini,
ambao familia yake ilikuwa tayari kwa kijana huyo kufanyiwa hilo zoezi
la upandikizwaji.
Wakati alipofika kwa ajili ya kufanyiwa
upasuaji huo wa kupandikizwa ini, iligundulika kuwa Ponnar anatatizo
katika mfumo wa upumuaji unaoitwa kitaalam Ebsteins
anomaly au kufeli kwa upande wa kulia wa moyo katika
kufanya kazi kwa usahihi ambao ndio awali umeletea udhoofu katika
ini.
Bahati mbaya
kujumuika kwa matatizo mawili kwa mpigo kulimfanya Ndg Ponnar kutokuwa
na njia mbadala yoyote mbali na kujumlisha upandikizaji wa ini
na moyo. Hii ni hatua ya upasuaji inayohusisha njia kuu mbili
kwanza ya kupitia kooni na kifuani (kwa ajili ya moyo) na kupitia
tumboni (kwa ajili ya ini) hivyo kufanya zoezi kuwa hatari
sana.
Ponnar- kwa
utulivu na ukakamavu alijiandaa kupigania uhai wake mpaka mwisho.
Familia yake hasa dada yake ambaye alikuwa tumaini na nguzo kwake,
maamuzi ya kwamba watafanya lolote liwezekanalo kuhakikisha wanamwokoa
kijana wao, walimpelekea hospitali za Apollo, Chennai,
India.
“kwa tatizo la
kuwa na moyo usiofanya kazi ipasavyo, kulikuwa na presha kubwa upande wa
nyuma wa ini iliyosababisha kuharikika kwa seli za ini iliyopelekea
udhoofu huo wa ini. Kwa kuongezea, timu ya upandikizaji wa ogani
walijadili uwezekano mkubwa wa uvujaji mwingi wa damu hasa kwa kuwa ni
upasuaji wa sehemu mbili kwa mpigo na pia uwezekano mkubwa wa sumu
kujikusanya kwenye ini, kuathiri moyo hasa kama ogani hizo mbili
zitapandikizwa tofauti tofauti” alisema ”Dk. Paul Ramesh,
mshauri mwandamizi wa upasuaji katika mfumo wa upumuaji kutoka hospitali
za Apollo,
Chennai.
Upasuaji na
upandikizaji wa moyo na ini unaweza fanyika kwa njia kuu
tatu;
Kwanza upandikizwaji wa moyo- ufuatiwe na
upandikizwaji wa ini kama njia mbili tofauti ila kwa mpigo katika
operesheni moja.
Upandikizwaji wa moyo na ini kwa pamoja,
inafanyika kwa ogani zote kuchukuliwa kama moja na kupachikwa kwa pamoja
kwa mpigo.
Ni wale mabigwa tu
kwenye ile timu ya upandikizwaji wa ogani kufanya kazi pamoja kama timu
moja na kuleta matumaini ya kufanikisha
CHLT mfumo adimu sana kufanyika
duniani.
”kwa zaidi ya
miongo ya ujuzi katika upandikizwaji wa ogani, imetuwezesha kupata
maarifa na utaalamu unaohitajika kufanya operesheni ngumu kama
hizi. Mafanikio yetu katika upandikizwaji wa moyo na ini yaliyopatikana
yametupatia msingi na uimara katika uendeshaji bora
wa CHLT kwa bara la Asia.
Najivunia sana kwa ajili ya Ponnar na familia yake walioweza kuimanini
timu kutoka hospitali yetu ya Apollo, imetupa sana motisha sisi
kuendelea mbele na mfumo huu bila mipaka ili kufika juu kabisa.
AliongezaDk.
Ramesh.
Ponnar alisubiri
kutokea April hadi 0ktoba 2015 ili mtoaji damu anayemfaa alipopatikana.
Alifanyiwa upasuaji wa upandikizwaji huo wa moyo na ini tarehe 14 oktoba
2015 na aliruhusiwa kwenda nyumbani ndani ya wiki baada ya upasuaji
huo. Leo hii, Ponnar ni mzima wa afya njiani kuelekea kupona kabisa na
kurudia maisha yake ya awali- ni mwenye furaha sababu ngozi yake sio ya
njano tena, na sasa anaweza kuendelea kufurahia raha za maisha kama
kutembea kwa miguu yake mwenyewe. Kwa maumivu yaliyokuwa nyuma kwa miaka
8, sasa Ponnar yupo huru kuendeleza matumaini yake na ndoto
zake.
Ngazi hii ya
kimatibabu, ya upandikizwaji wa moyo na ini kwa mpigo (mara ya kwanza
barani Asia) ni hazina kubwa kwa Ndg Ponnar na dada yake,walioweza
kutosikiliza uzushi wa watu wote. Pia ni ushuhuda kuwa timu ya madaktari
wa upandikizwaji kutoka hospitali za Apollo Chennai wamefanikiwa
kufanya operesheni hii kwa mafanikio makubwa. Haya yote yasingeweza
kufanikiwa kama pia kusingekuwepo kwa ushirikiano mkubwa kutoka serikali
ya Tamilnadu na programu ya kujitolea ogani iliyopo Tamilnadu ambayo
imesifiwa ulimwenguni kwote kwa kazi kubwa
walioifanya.
”mafaniko haya
makubwa ni agano kwa mabingwa wote wa upasuaji duniani, madaktari,
wataalam, manesi na wafanyakazi wote waliojitolea kuwahudumia wagonjwa
na kutoa huduma zilizopo katika viwango vya kimataifa. Upasuaji ni
matokeao ya mipango bora iliyofanywa kwa siku kadhaa kutoka kwa timu ya
wataalam upande wa moyo na ini na uonekanaji wa miundo mbinu bora na
wataalam waliokubuhu. Jitihada hizi shirikishi zinachukua timu zote za
upandikizaji ili kutathimini na kuweka mikakati kasha kuonyesha kuwa
fani hii ni ya kuheshimika”. Alisema Dk. Prathap C
Reddy, mwenyekiti na mwanzilishi wa Hospitali za
Apollo.
Hospitali ya Apollo
ilifunguliwa mnamo mwaka 1983, na kutoka kipindi hicho imekuwa
ikiendeshwa kwa kauli mbiu isemayo "Dhamira yetu ni
kuleta huduma ya kisasa karibu kabisa na walengwa. Tunajitolea kutoa
huduma bora na mafanikio katika elimu na utafiti kwa ajili ya
jamii ya
kibinadamu".
Katika miaka 30 tokea
kuanzishwa kwake, hospitali ya Apollo imeandika historia kubwa kupata
kuonekana nchini India. Ni moja ya kampuni kubwa ya Afya katika bara la
Asia, na pia imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya afya nchini
india.
Katika safari yake,
imeweza kuboresha maisha ya watu wapatao milioni 39 kutoka nchi
120.Inatoa huduma maalum 52 na vitanda vya upasuaji 710.Imefanya
upasuaji wa moyo wenye kufikia idadi ya watu 152,000 na panuzi 125, 000
za mishipa myembamba.Imefanya upasuaji wa wa viungo unaopita kiasi cha
idadi ya watu 10,000, upasuaji wa uvimbe wa ubongo, uti wa mgongo na
zaidi.Taasisi ya Apollo ni moja ya taasisi zinazoongoza nchini india,
zikiwa na teknolojia za kisasa kama Novalis TX, PET MRI na Upasuaji
unaotumia mashine za kiroboti.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni