.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 18 Desemba 2015

JOSE MOURINHO ATIMULIWA CHELSEA

         Kwaherini Chelsea, lakini mpo moyoni mwangu. Jose Mourinho pichani. 

Timu ya soka ya Chelsea imemtimua kocha wake Jose Mourinho baada ya pande zote mbili, yaani uongozi wa timu na kocha huyo Mreno kufikia maridhiano. 

Kufutwa kazi kwa Mourinho kunafuatia matokeo mabovu ya mabingwa hao watetezi wa ligi kuu England ambao mpaka sasa katika msimamo wa ligi Chelsea wapo nafasi ya 16. 

Hii ni mara ya pili kwa Mourinho aliyejiunga na Chelsea mwaka 2013 kutimuliwa na klbabu hiyo ya Ungereza. 

Mourinho ni mmoja wa makocha waliopata kupendwa kupitwa kiasi na mashabiki wa Chelsea wa England na nje ya nchi hiyo. Hata kufukuzwa kwake, wengi wa mashabiki wameonekana kuumia na kuanza kuitabiria mabaya zaidi timu hiyo.

Pia ndiye kocha aliyeipa mafanikio makubwa timu hiyo, lakini msimu huu mambo yameonekana kumuendea kombo, huku kukiwa na tetesi kwamba amekuwa akihujumiwa na baadhi ya wachezaji wake nyota.
                      Wakati ni mgumu jahazi linaenda mrama benchi lote kimyaaaa
                         Wakati wa furaha baada ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu England
                                                               Je Chelsea wanamtaka Pep Guardiola
                                                                                                          Au Guus Hiddink




Hakuna maoni :

Chapisha Maoni