Na Shushu Joel,Busega
Ugonjwa umepiga hodi jana jioni kwa
mgonjwa mmoja mkazi wa kata ya Lamadi kuzidiwa na kupelekwa katika
hospital ya mkula iliyo chini ya kanisa na hivyo kuweza kufungulia
njia kwa wengine kwa sasa wagonjwa wanazidi kuongezeka na huku wala
hakuna eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya wagonjwa hao.
Hali inavyoonyesha uenda ugonjwa huo
ukaitesa zaidi wilaya hiyo na hii ni kutokana na wakazi wengi wa
maeneo hao kutokuwa na vyoo hasa kando mwa Ziwa Victoria maeneo kama
Buyolwa ndogo ambako wakazi walio wengi wanajisaidia katika msitu
ulio umbali wa mita chache na ziwa ambalo ndio kiungo kikubwa katika
eneo hilo kwani maji utumika kwa shughuli zote za viumbe hai
zinazohitajika kutumika.
Wakizungumzia juu ya ugonjwa huo
wananchi wa busega wanawatupia lawama watumishi wa afya kwa kusema
kuwa wao ni sababu ya kuingia na kueneo kwa ugonjwa huo wilaya humo
kwa kusema kuwa wanapoenda kukagua maeneo machafu wanashindwa
kuchukua maamuzi ya kuwafungia wahusika hao.
Luge Elikana mfanya biashara wa
samaki toka katika mwalo wa Buyolwa ulioko kata ya kiloleli anasema
kuwa watu zaidi ya 200 ukutana katika mwalo huo asubui kwa ajili ya
biashara ya samaki lakini tatizo lililopo hapa ni ukosefu wa vyoo
katika majumba ya watu na hata magesti ya eneo hilo.
Aliongeza kuwa kwa upande wa gesti
ni hatari sana endapo milipuko hii ikiendelea kwani vyumba nui vidogo
na pia hazifai kwa matumizi ya mwanadamu hivyo lawama ni kwa uongozi
wa afya.
Akitoa taarifa za uwepo wa ugonjwa
huo Mganga Mkuu wa wilaya Hiyo Godfrey Mbagali alisema kuwa ni kweli
ugonjwa huu umetufikia Busega lakini tumesha fanya mikakati kabambe
ya kuhakikisha ugonjwa huu ausambai kwa wananchi ili kuweza kuokoa
maisha ya wananchi wote.
Aliongeza kuwa mpaka sasa tumepokea
wagonjwa 8 tu na wote wameshapata huduma sitahiki na wako katika
uangalizi mkali wa wataalamu wa afya lakini tunamshukuru mungu hali
zao zinaendelea vizuri.
Aidha Mbagali aliwataka wananchi
wote kuweza kuzingatia yale aliyokuwa akiyasema kipindi cha nyuma
ambapo aliwaasa wananchi kuchemsha maji ya kunywa,kunawa mikono
wanapotoka kujisaidia na kuongeza usafi zaidi majumbani kwani hii
itasaidia kutosambaza maambukizi kwa watu wengine.
Alisema kuwa kuanza juzi tumeanza
tena kutoa matangazo kwa wananchi wote ndani ya wilaya kuwakumbusha
jinsi ya kuzingatia usafi na kuepukana na ugonjwa wa kipindupindu pia
aliwaambia wananchi watambue kuwa ugonjwa huu ni hatari.
MWISHO
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni