Hali hii ni tofauti kwa vijijini ambapo wananchi wengi mwenendo wa maisha yao ya kila siku kutoka kwa viongozi wao kuanzia ngazi ya kijiji, kitongoji na kata. Kutokana na aina hii ya maisha inawafanya wawe na umoja, kuishi kwa ushirikiano na kufanya maamuzi kwa pamoja hasa juu ya rasilimali zao.
Katika miaka ya hivi karibuni anakijiji wengi wanaoishi katika maeneo yenye
rasilimali wametambua umuhimu wa kutunza na kutumia rasilimali zao vizuri kwa maendeleo yao na kwa manufaa ya vizazi vijavyo. Lakini si kila sehemu hali ipo hivyo katika baadhi ya maeneo wanakijiji wamekuwa hawazitambui haki zao za msingi kutokana na uelewa mdogo.

Mwime ni kijiji kilichopo katika kata ya Mwendakulima wilayani Kahama, mkoani Shinyanga. Wakazi wengi wa kijiji hiki ni wakulima wadogo wadogo, wafugaji na ni wachimbaji wa madini.
Kijiji hiki ndicho kilichohifadhi mgodi maarufu wa dhahabu wa Buzwagi, uliochangia kwa kiasi kikubwa kupanda kwa hadhi ya kijiji hicho na kuwa mtaa. Hivyo kwa sasa Mwime ipo kwenye halmashauri ya mji kutokana na upatikanaji wa huduma muhimu karibia zote kuanzia huduma za afya, barabara, umeme na maji safi.
Awali kijiji cha Mwime kilikuwa kikimiliki leseni mbili za machimbo ya uchimbaji dhahabu ya Majimaji na Zanzibar.
Wachimbaji wadogo wadogo walikuwa ndio walengwa wakubwa, ambapo walilipa ushuru kwa serikali ya kijiji. Na wao kunufaika na shughuli hizo ambazo zilikuwa zinawaingizia kipato.
Malipo haya yalitakiwa kuanza kulipwa kuanzia mwaka
2009 miaka miwili baada ya makubaliano kusainiwa tarehe 21 mwezi Aprili mwaka 2007. Ni mwaka 2012 malipo haya yamelipwa kwenye akaunti ya kijiji, kiasi hicho cha shilingi milioni 300/- ni malipo ya miaka mitano ya awamu ya kwanza; mkataba unatamka kila baada ya miaka 5 pande mbili (Kijiji na Mgodi) zitakaa kupitia kiwango hiki ili kuboresha kiwango hiki kutegemeana na uzalishaji. Malipo haya yanafanyika, baada ya juhudi kubwa kufanywa na wananchi wa kijiji cha Mwime na viongozi wao katika kufuatilia fedha hizo.
Na tatizo halikuwa upande wa mgodi wa Buzwagi, bali ni wananchi wa kijiji cha Mwime wenyewe kushindwa kuhimiza uongozi wao kuchukua hatua za kufuatilia suala hilo. Na hivyo kupita miaka miwili bila kitu chochote kufanyika kuanzia 2009 hadi 2011.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni