Papa Francis amewaonya waumini
bilioni 1.2 wa kanisa hilo duniani kutokubali kuingiwa na sumu ya
kupenda kujilimbikizia mali mno, katika ujumbe wake wa Krismasi.
Akiongea kwenye ibada ya mkesha wa
Krismasi la Mtakatifu Peter, Basilica, Papa Francis amewataka waumini
kuishi maisha ya kawaida yenye kuzingatia upendo, usawa na
kusaidiana, ambayo si ya ubinafisi na kuongozwa na tamaa ya
kujilimbikizia mali.
Baadae hii leo Papa Francis atatoa
ujumbe wake wa Krismasi kama ilivyo kwa tamaduni za Kanasa Katoliki,
akiwa eneo la balkoni eneo la kwenye uwanja wa Mtakatifu Peter.
Papa Francis akibusu mdoli wa mfano wa mtoto Yesu katika ibada kwenye kanisa la Mt. Peter, Basilica
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni