Rais wa Sri Lanka amesema kuwa
waandaaji wa tamasha la Enrique Iglesias, wanapaswa kupigwa bakora
kutokana na tabia isiyofaa iliyoonyeshwa na baadhi ya mashabiki
wanawake katika tamasha hilo.
Rais Maithripala Sirisena amesema
picha za baadhi ya wanawake walioonekana wakimkimbilia Iglesias na
kumbusu pamoja na kumrushia nguo zao za ndani si za kistaarabu hata
kidogo.
Rais Sirisena amesema waandaaji wa
tamasha la Enrique Iglesias wanapaswa kuchapwa na mijeledi wenye vitu
vya kuchoma, akimaanisha adhabu kali iliyokuwa ikitoolewa katika mika
ya kale.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni