Rapa Kanye West na Mkewe Kim
Kardashian wameanza ukarabati eneo la shamba la zabibu lililopo eneo
la Hidden Hills, California katika kujipanga kuanza kufanya biashara
ya kutengeneza mvinyo.
Kwa miezi 16 iliyopita wanandoa hao
wamekuwa wakikarabati jengo lao lenye thamani ya dola milioni 20
lililopo kwenye eneo hilo, katika kujaribu kuongeza kuboresha
mazingira ya eneo la futi 20,000.
Pamoja na hayo Kim, na Kanye,
wanashauriana na wataalam kuhusiana na namna watakavyoweza kulitumia
shamba la mizabibu la hekari 3 ambalo halijaendelezwa katika kuweza
kuzalisha mvinyo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni