.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 4 Desemba 2015

RC MAKALA AKUNWA NA MATOKEO MAZURI YA DARASA LA SABA WILAYANI HAI

Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Amos Makalla, akiwa ameshika glasi ya kinywaji kwa ajili ya kufurahia kwa pamoja kwenye hafla ya kuwapongeza walimu wa wilaya ya Hai mkoani humo baada ya kupata matokeo mazuri katika ufaulu wa darasa la saba mwaka huu. Hai imeshika nafasi ya kwanza kiwilaya mkoani humo na nafasi ya nne kitaifa.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Amos Makalla, mwenye suti nyeusi akiingia katika hafla hiyo, wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro. 

                                                                                   Na Mwandishi Wetu, Hai

MKUU wa Mkoa Kilimanjaro, Amos Makalla, amehudhuria halfa ya kuwapongeza walimu wilayani Hai, mkoani humo, kwa kufanikisha ufaulu mzuri wa darasa la saba. Wilaya ya Hai imepata nafasi ya kwanza kiwilaya mkoani Kilimanjaro, huku ikishika ikishika nafasi ya nne kitaifa, jambo lililomkuna Mkuu huyo wa Mkoa Kilimanjaro.
 

Akizungumza katika halfa hiyo akiwa kama mgeni rasmi, RC Makalla, alisema kwamba Hai wanastahili pongezi na wanapaswa kuendelea kufanya bidii ili wazidi kufaulisha kiwilaya na kitaifa. Alisema kuna haja ya sekretarieti ya Mkoa huo na Halmashauri zote kujipanga na kushughulikia kero za walimu, madai ya mishahara, kupandishwa kwa madaraja pamoja na kujibu barua zao kwa wakati ili kuwapa moyo walimu wao hao.

“Mkoa wetu unawapa pongezi kubwa walimu wote wa wilaya ya Hai kwa kufanya kazi kubwa na nzuri ya kuhakikisha kwamba wanafunzi wenu wanafaulu vizuri. “Naomba muendelee kujituma katika ufundishaji wenu, huku nikiahidi ushirikiano mkubwa katika ofisi yangu na kwenu ninyi walimu ili kuleta ushirikiano mkubwa kati yetu,” alisema.

RC Makalla amekuwa akifanya ziara mbalimbali mkoani Kilimanjaro ili kuongeza ufanisi katika majukumu yao ya kila siku, huku wakiitumia vyema falsafa ya Hapa Kazi Tu, inayotumiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni