.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 4 Desemba 2015

WALIOCHOMA MOTO KITUO CHA RADIO, HITS FM WASAKWE NA KUCHUKULIWA HATUA KALI

Mmiliki wa Redio Hit Fm Mohammed Abdalla akiongozana na Viongozi waliotembelea Studio yao na kujionea uharibifu uliotokea kwa moto huo.
( Picha kwa hisani ya ZanziNews )

Rweyunga blog ina imani na jeshi la polisi, na kuliomba jeshi hilo liwasake wahusika wote waliokichoma moto kituo hicho bora cha matangazo visiwani Zanzibar na kwachukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria za nchi. 

Aidha Rweyunga blog inampa pole mmiliki wa kituo hicho pamoja na uongozi na wafanyakazi wote.
Waandishi na Wananchi waliofika kujionea moto uliounguza kituo hicho cha Redio cha Hit Fm kilichoko migombani Zanzibar.
 Mwandishi akimuhoji Mkuu wa Utawala wa Afisi Kuu ya CCM alipofika kuangalia kituo hicho cha Hit Fm kujionea hasara iliopata kituo hicho
Mmiliki wa Kituo hicho cha Hit Fm Mohammed Abdalla Mohammed akizungumza na waandishi wa habari kutokana na hasara aliyoipata kwa moto huo na kulaani kitendo hicho cha kutiliwa moto studio yake na kuweza kupata hasara kutokana na kuunguwa kwa vifaa vya studio hiyo.
Meneja wa Redio ya Hit Fm Hafidh Kassim akizungumza na waandishi wa habari hasara walipata kutokana na moto huo na kukosa kuwa hewani kwa matangazo yake kama kawaida. Na kulaani kitendo hicho cha kuchomewa Studio yao kimefanya kuwakosesha ajira Wafanyakazi wa Kituo hicho.
Mkuu wa Atawala wa Kampuni ya Zanzibar Cable akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali viliko Zanzibar kuhusiana na janga hilo la kuchomwa kwa Kituo cha cha Redio cha Hit Fm na kusababisha hasara ya shilingi karibu milioni 65 kwa kuugua kwa vifaa vya utangazaji katika studio hiyo, wakayi ikiwa hewa na kuvamiwa na Watu wasiojulikana, katika ajali hiyo wafanyakazi wamepata majaraha.
Waandishi wakifuatilia kwa makini maelezo yanayotolewa na Mkuu wa Utawala Kampuni hiyo inayomiliki Kituo hichi Zanzibar Cable akitowa maelezo ya hasara iliopatikana kutokana na kuungua kwa Studio hiyo.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar wakifuatilia taarifa hiyo ya ajali ya moto ya Kituo cha Redio cha Hit Fm kutiwa moto na Watu wasiojulikana.
Meneja wa Baraza la Habari Tanzania MCT Zanzibar Suleiman Seif akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kuhusiana na kutiwa moto kituo cha Redio cha Hit Fm Zanzibar na Watu wasiojulikana usiku wa manani juzi 2 disemba.2015, kushoto mtangazaji wa kituo hicho.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni