Meza kuu,wa kwanza kulia ni Meneja wa redio PANGANI FM Maimuna Msangi, wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi wa shirika la UZIKWASA ambalo limeratibu tamasha hilo VERA PIEROTH,wa tatu ni Kaimu mgeni Rasmi ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya PANGANI Bi Patricia, na wanne ni Mratibu wa masuala ya UKIMWI wilaya ya PANGANI.
Mkurugenzi wa shirika la UZIKWASA, VERA PIEROTH akizungumza jambo wakati wa kuwakaribisha wananchi wa PANGANI katika tamasha hilo.
Kaimu mgeni rasmi ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii Bi.Patricia akizungumza na wananchi waliohudhuria katika tamasha hilo.
Burudani ya ngoma ilikua sehemu ya tamasha hilo.
Washehereshaji wa tamasha hilio, Pili Mlindwa na Shabani Kizamba wakiwajibika.
Mkurugenzi wa shirika la Uzikwasa na Meneja wa Pangani FM.
Wanakamati wa kijiji cha Mseko katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa washindi, na wameibuka washindi kwa mwaka wa 3 mfululizo.
Mmoja wa wanakamati ya VMACK ya kijiji cha mseko akicheza kwa furaha mbele ya meza kuu baada ya kutangazwa washindi,
Kaimu Mgeni rasmi Bi.Patricia akiwa ameshika ngao ambayo ni zawadi ya washindi wa VMACK kwa mwaka 2015.
Katibu wa kamati hiyo akipokea zawadi, Ngao na Hundi ya shilingi laki sita.
Vijana bora wa mfano wa kuigwa walioingia katika hatua ya 3 bora, na aliyeibuka mshindi ni kijana aliyevaa tshirt rangi ya njano.
Wamama walioingia katika tatu bora mama mfano wa kuigwa, na aliyeibuka mshindi ni mama ambaye ameshikilia pochi, ambaye anajulikana kwa jina maaarufu kuti kavu.
Hapa akipokea zawadi ya hundi ya shilingi laki 1 kwa kua mama/mwanamke bora mfano wa kuigwa kwa mwaka 2015.
Mwenyekiti wa kijiji cha Jaira akigawa zawadi ya sare za shule kwa viongozi wa vijiji vyote vya Wilaya ya PANGANI kwa niaba ya Aliyekua kijana bora mfano wa kuigwa mwaka 2013-2014,ambayo aliahidi kwa watoto yatima alipochaguliwa.
Wamama wakifurahia jambo.
Sehemu/baadhi ya wananchi waliohudhuria katika tamasha la kuzizawadia kamati bora za kudhibiti UKIMWI, kijana bora na mama bora wa mfano wa kuigwa kwa mwaka 2015 zilizofanyika katika kijiji cha JAIRA kata ya MADANGA Wilayani PANGANI.
Waandishi wa habari kutoka redio PANGANI FM, iliyochini ya shirika la UZIKWASA wakifuatilia kwa makini tamasha hilo (waliovaa tshirt za PANGANI FM).
Wananchi wa Pangani waliofika katika kijiji cha Jaira wakifuatilia kwa ukaribu tamasha hilo.
Na Mwandishi wetu
Shirika
lisilo la kiserikali Wilayani Pangani la UZIKWASA linalojishughulisha
na kuziwezesha kamati za kudhibiti Ukimwi, VMACK limezawadia kamati bora
za kudhibiti ukimwi Wilayani humo.
Sherehe hizo zimefanyika sanjari na kuwazawadia kijana bora mfano wa kuigwa na mama bora mfano wa kuigwa.
Katika
sherehe zilizofanyika kijiji cha Jaira,K ata ya Madanga wilayani
Pangani na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wananchi na viongozi
kutoka halmashauri ya Wilaya ya Pangani mgeni rasmi alikuwa Kaimu Afisa
Maendeleo Wilaya ya Pangani, Bi.Patricia Kinyange.
Akizungumza
katika hadhara hiyo Bi. Kinyange amelipongeza shirika hilo kwa
kuzijengea uwezo kamati hizo ambazo zinafanya kazi kubwa kwa jamii.
“Kwa
kweli shirika la UZIKWASA nawapongeza sana, mnafanya kazi kubwa kwenye
jamii ya Pangani na kwakweli watu wa Pangani wanapaswa kujivunia uwepo
wenu. Nimeshangaa kuona mambo makubwa yanayofanywa na kamati kutokana na
elimu mnayowapatia,mnastahili pongezi kubwa”alisema Bi.Kinyange.
“Mfano
mzuri mimi ARUSHA nilipokua nafanya kazi, kamati zipo lakini kwakweli
wamelala,unakuta kamati inakutana mara mbili kwa mwaka mzima,lakini huku
ni zaidi ya mara kumi,kwakweli nimeshangaa sana,nyinyi ni shirika
ambalo linafaa kuigwa,lakini wanakamati niwaombee mzidishe juhudi
msiwaangushe wanauzikwasa na sisi kama halmashauri tutajitahidi
kushirikiana kwa karibu kabisha na UZIKWASA ili kuendeleza juhudi hizi.”
Katika
hatua nyingine mgeni huyo rasmi amempongeza kijana aliyeibuka mshindi
katika shindano la kijana bora mfano wa kuigwa na kumtaka kuendeleza
juhudi zake na kwamba Halmashauri watamtumia kama darasa kwa ajili ya
vijana wengine kujifunza kutoka kwake.
Kwa upande wao kamati
iliyoibuka mshindi kwa mwaka wa tatu mfululizo kutoka katika kijiji cha
Mseko wamesema umoja na mshikamano ndio nguzo pekee ya ushindi wao,na
kwamba shukrani pekee zinapaswa kwenda kwa UZIKWASA kwa mafunzo na
ufuatiliaji wao kwani ndio vilivyowafanya kutekeleza mipango
waliojiwekea kama wanakamati hadi kuibuka washindi.
‘Naweza
kusema kamati yetu imejitoa sana,wanakamati wanatumia muda wao mwingi wa
ziada katika kuhakikisha tunatekeleza mipango tuliojiwekea,lakini pia
msukumo mkubwa ni kutoka UZIKWASA kwakweli tunawashukuru sana”Alisema
Afisa mtendaji mseko.
Kwa upande wake Mratibu wa shughuli hizo
kutoka shirika la UZIKWASA ambaye pia ni Afisa wa mradi wa jinsia na
uongozi wenye mabadiliko, Bi.Salvata Kalanga amesema haikuwa kazi rahisi
kuzipata kamati bora 8,kutokana na ushindani mkubwa uliokuwepo kwa
washiriki 15,lakini wanashukuru kumpata mshindi ambaye wanaamini
anastahili kutokana na kazi waliyoifanya.
Katika sherehe
hizo,mshindi wa kwanza amepata zawadi ya ngao,pamoja na fedha taslimu
shilingi laki sita,mshindi wa pili alipata laki 4 na nusu,na mshindi wa
tatu alipata shilingi laki 4.
Sherehe ya kuzizawadia kamati bora
za kudhibiti UKIMWI hufanyika kila mwaka chini ya shirika la
UZIKWASA,lengo ni kuzipa motisha kamati hizo ili zifanye vizuri zaidi.
Mashindano
haya na tamasha hili husimamiwa na kuwezeshwa na Asasi ya UZIKWASA
Pangani kwa lengo na Kuamsha hamasa, kuchochea, kutafakari na kujifunza
na kujenga uwajibikaji miongoni mwa vijana, akinamama na Kamati za
Kudhibiti UKIMWI jinsia na uongozi za vijiji.
Mashindano haya
huanza baada ya UZIKWASA kuwezesha kamati hizi kwa kuzijengea uwezo na
baadae maafisa wa UZIKWASA kuzitembelea kamati hizo na makundi
yaliyotajwa na kupima utekelezaji wake kwa kuzingatia vigezo
vilivyowekwa na kukubaliwa na wadau hao.
Kamati, vijana, na akina
mama walioanishwa kufanya vizuri hutembelewa na kamati nyingine kuweza
kujifunza kwa pamoja na kujirudhisha kwa utekelezaji wa kamati hizo. Pia
kwa vijana na wakinamama hutembeleana na kupeana taarifa za utekelezaji
na kujifunza kwa pamoja. Kamatai hizo na hao vijana na akinamama
huchujwa na kubaki wachache ambao wanatekeleza vizuri zaidi.
Baada
ya zoezi hilo la kutembeleana walioanishwa huitwa Pangani na
kukutanishwa na waamuzi ambao huwasikiliza na kuchambua washindi.
Mwaka
2015 kamati 12 zilichaguliwa kuingia kwenye ushindani huo ambazo ni
Mseko, Mwembeni, mkwajuni, mbulizaga, Bweni, mzambarauni, Mtonga,
Mikocheni, Langoni,Tungamaa, Sange na Jaira.
Akina mama bora
waliongia sita bora kati ya 33 ni kutoka Masaika, Kwa kibuyu, Stahabu,
Mwembeni, Mtonga na Langoni. (watatu watazawadiwa)
Vijana bora waliongia sita bora kati ya 33 ni kutoka Msaraza, Kimanga, Mikocheni, Mseko, Boza na Mivumoni.(watatu watazawadiwa).
Mashindano
haya yalianzishwa mwaka 2010 ili kuleta msukumo, ushindani na chachu ya
utekelezaji wa mipango ya vijiji ya ukimwi na maendeleo ya kijiji kwa
ujumla na kuotesha mbegu ya uwajibikaji.
Mwaka 2010 Kamati ya
Sanga iliibuka mshindi, mwaka 2011 kamati ya Langoni, iliibuka mshindi,
mwaka 2012 kamati ya Langoni iliibuka mshindi tena. Mwaka 2013 kamati ya
Mseko iliibuka mshindi na mwaka 2014 Mseko iliibuka mshindi tena.
Mwaka
huu wa 2015 mchuano ulikuwa mkubwa na kamati zimejituma na kuwajibika
katika utekelezaji wa mipango yao ya maendeleo pamoja na kuyasaidia
makundi mbalimbali yenye uhitaji.
Kamati kumi 15 zimetekeleza
vizuri. Kamati 12 zimetekeleza wastani. kamati 6 ikiwepo, Ushongo,
Kipumbwi, Masaika, Kigurusimba, kimang,a na Mivumoni zinahitaji msukumo
wa ziada kwa Kukosa uwajibikaji.
Mashindano haya yameleta
msukumo katika shughuli zote za kiuongozi na maendeleo ya vijiji.
Palipo na uongozi mzuri na utekelezaji mzuri unakuwepo pia.
UZIKWASA
itaendelea kuwajengea uwezo viongozi wangazi zote na wanajamii kuweza
kujitathmini, kuzama na kujichunguza na kuweza kufanyia kazi changamoto
za kiuongoza na kuwezesha maendeleo katika jamii. Suala la kupinga
unyanyasaji wa wanawake na watoto wa kike litapewa kipaumbele.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni