Balozi Mahiga akiagana na Mgeni wake.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga amefanya mazungumzo leo na Waziri wa Nchi wa Mambo ya Nje wa Japan, Mhe. Seiji Kihara ambaye aliwasili nchini jana kama Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Japan Mhe. Shinzo Abe ambapo kesho tarehe 16 Desemba 2015 anatarajiwa kuwasilisha Ujumbe wa Waziri Mkuu wa Japan kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk. John Pombe Joseph Magufuli.
Pamoja na kuwasilisha ujumbe kwa Mheshimiwa Rais,
mgeni huyo anatarajiwa kuhudhuria hafla
ya utiaji saini wa mkataba wa mkopo wa dola za kimarekani
milioni 96 utakaotolewa na Serikali ya Japan kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirishia umeme wa
Kenya na Tanzania wenye urefu wa kilometa 441.5 kutoka Singida na
Manyara kupitia Babati na Arusha mpaka
Namanga.
MAHUSIANO KATI YA TANZANIA NA
JAPAN
Tanzania na Japan zimekuwa katika uhusiano na ushirikiano wa
karibu mara tu baada ya Tanzania kupata uhuru wake. Mahusiano hayo
yamekuwa yakikua na kuimarika miaka hadi miaka katika nyanja mbalimbali
ikiwemo miundombinu, afya, nishati, Kilimo, biashara, viwanda,
usafirishaji na uwekezaji.
Kufanyika kwa ziara hii ya Waziri
wa Nchi wa Mambo ya Nje wa Japan ni muendelezo wa kukuza ushirikiano
baina ya nchi zetu mbili.
Serikali imeingia makubaliano na Serikali
ya Japan kutekeleza miradi mitatu ya ujenzi wa barabara yenye lengo la
kupunguza tatizo la msongamano wa magari jijini Dar es Salaam
linaloathiri uchumi wa nchi yetu. Miradi hiyo ni pamoja
na:
Mkataba wa ujenzi wa Barabara hiyo tayari
ulikwishasainiwa tangu tarehe 15 Oktoba 2015 na ujenzi unategemewa
kuanza mapema mwakani.
Mradi ya Ujenzi wa Barabara ya Morocco –
Mwenge
Serikali ya Japan itafadhili upanuzi wa
barabara ya Mwenge – Morocco ili kuweza kupunguza msongamano wa
magari.Upanuzi wa barabara hii nao unatarajiwa kuanza
mwakani.
Tayari Serikali imekwishaanza hatua za mwanzo za
ujenzi wa barabara hiyo kufuatia uamuzi wa Mhe. Rais kuelekeza fedha
zilizokuwa zigharamie sherehe za uhuru zitumike kuanza kazi ya upanuzi
wa barabara hiyo.
Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Gerezani
mpaka bendera tatu
Mradi huu unatarajiwa kutekelezwa kwa
fedha za msaada kutoka Serikali ya Japan. Ujenzi wa barabara hii nao
unatarajiwa kuanza mwakani.
Mbali na miradi ya ujenzi wa barabara,
Serikali ya Japan imeingia makubaliano na Serikali ya Tanzania
kutekeleza miradi ya umeme kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa umeme wa
kutosha kwa matumizi ya wananchi na viwandani kama ilivyoahidiwa kwenye
ilani ya uchaguzi ya CCM.
Miradi
itakayotekelezwa kwa ufadhili kutoka Japan ni pamoja
na:
Mradi ya Ujenzi wa Njia ya Kusafirishia
Umeme Kenya – Tanzania Power Interconnection
Project
Mradi huu una lengo la kuimarisha
usambazaji kwa kuuza na kununua umeme katika nchi za Jumuiya
ya Afrika Mashariki hasa Kenya. Ni ujenzi wa njia ya kusafirishia umeme
wenye KV400 na urefu wa kilomita 414.5 kutoka Singida na Namanga kupitia
Babati na Arusha.
Mkataba wa mradi huu unatarajiwa kutiwa
saini baadaye leo Wizara ya Fedha na kushuhudiwa na Waziri wa Nchi
wa Mambo ya Nje wa Japan
Mkataba wa ujenzi wa Mitambo ya kuzalisha
umeme wa MW 300 huko Kinyerezi ulisainiwa tarehe 27 Machi 2015
kati ya Serikali na Benki ya Kimataifa ya Ushirikiano wa Kimaendeleo ya
Japan (Japan Bank for International Cooperation – JBIC).
Utekelezaji wa Mradi huu unatarajiwa kuanza mapema mwakani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni