.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 17 Januari 2016

BAADA YA KUFIWA NA MUMEWE CELINE DION APATA MSIBA MWINGINE WA KAKA

Mwanamuziki raia wa Canada, Celine Dion amefiwa na kaka yake mkubwa aliyekuwa akiugua saratani, siku chache tu kupita tangu afiwe na mumewe kwa ugonjwa wa saratani ya koo.

Kaka huyo wa Dion, Daniel Dioni, 59, amefariki dunia jana karibu na Jiji la Montreal huko Canada, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa mwanamuziki huyo.

Familia ya Dion amemuelezea Daniel Dion ambaye alikuwa ni baba wa watoto wawili kuwa ni mtu mkarimu, asiye na mijivuno na ambaye alibarikiwa kuwa na vipaji vingi.

Mume wa Celine ambaye pia aliwahikuwa meneja wake, Rene Angelil, 73, alifariki dunia siku ya Alhamisi, nyumbani kwake Las Vegas, Marekani.
            Celine Dion akiwa amekumbatiana na mumewe marehemu Rene Angelil

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni