.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 30 Januari 2016

BONDIA OMARI KIMWERI KUPANDA TENA UWANJANI FEB 26 AUSTRALIA


BONDIA mzaliwa wa Tanzania Omari Kimweri ambaye ni bingwa wa uzito wa flyweight nchini Deer Park, Victoria, Australia anatalajia kucheza mpambano wake mwingine feb 26 akizipiga na Michael Camellion kutoka Philippinesa mpambano wa raundi kumi ubingwa wa WBA Pan African light flyweight title utakaopigwa katika ukumbi wa

The Melbourne Pavilion, Flemington, Victoria, Australia

Kimweri mpaka sasa amepanda uringoni mara 17 tangia aanze kucheza ngumi za kulipwa mwaka 2007 akiwa ameshinda michezo 14 na kupoteza michezo 3

Bondia huyo mtanzania anaefanya shughuli zake huko amewaomba watanzania kumuombea duwa kwa ajili ya mpambano huo ili afanye vizuri mana akishinda mchezo huo

Atakuwa na uwezo wa kupigania ubingwa wa Dunia wa WBA

Kwa kuwa maandalizi anayoyafanya kwa sasa ni mazuri na sapoti anayoipata ni nzuri sana , na akishinda mchezo uho itabadilisha maisha ya mchezo wake wa masumbwi na kuwa na kipato kikubwa wakati akipigania mikanda mikubwa inayotambulika Duniani akianzia na mkanda wa WBA ambao ameaidiwa kucheza baada ya kushinda mechi yake hii ya feb 26

Kimweri alitoa shukrani za kumsapoti kwa makocha wa Tanzania aliokwisha fanya nao kazi ambapo mpaka sasa anawakumbuka kwa mchango wao mkubwa katika mchezo wa masumbwi ni Baba yake mzazi Idd Kimweri, kaka yake Riadha Kimweri, Habibu Kinyogoli , Rajabu Mhamila 'Super D'

Kocha wa Tanzania Prison Remmy Ngabo,Kameda Antony pamoja na mabondia wa mkoa wa Tanga na Antony Edoa pamoja na kaka zake wote katika mchezo wa masumbwi Twalib Kimweri Mzonge Hassan, Ibrahimu Mashi, na mama zake wote kutoka mkoa wa Tanga , ambao amekuwa chachu katika mchezo wa ngumi mpaka amefikia hatua ya kuwa hapo alipofikia na ata kama anaishi nje ya Tanzania ato sahau asili yake kwa kuwa kitovu chake ndipo kilipozikiwa
 
 
Mwanasoka wa kike, Melanie Gines ambaye ni raia wa Hispania (kushoto) akimkabidhi vifaa vya mchezo wa masumbwi kocha wa Rajabu Mhamila 'Super D' baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam, mwaka jana walipotembelea nchini
 Mwanasoka wa kike, Melanie Gines ambaye ni raia wa Hispania (kushoto) kocha Rajabu Mhamila 'Super D' baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam, mwaka jana walipotembelea nchini

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni