.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 20 Januari 2016

GEORGE CLOONEY NA LUPITA NYONG'O WAZUNGUMZIA MVUTANO WA TUZO ZA OSCARS

George Clooney ametoa ya moyoni juu ya uteuzi wa waigizaji filamu wote weupe katika tuzo za Oscars, hali iliyojitokeza kwa mwaka wa pili mfululizo na kuwabania waigiazaji wenye asili ya Afrika.

Clooney mmoja wa waigizaji filamu nguli, amesema ghafla tumeanza kuelekea katika mueleko usio sahihi, na kuongeza kuwa kunawatu waliopaswa kuteuliwa kuwania tuzo hizo ambao hawapo.

Clooney mshindi huyo wa tuzo ya Oscar mara mbili amesema mwaka huu waandaaji wa tuzo za hizo wamezipamgongo filamu ya nyota Will Smith ya Concussion, ya Idris Elba ya Beasts of No Nation, Creed pamoja na Straight Outta Compton kama filamu bora.

Kilio hicho pia cha kutopewa watu weusi kuwania tuzo zote muhimu za filamu za Oscars pia kimemgusa mshindi wa tuzo ya Oscar Lupita Nyo'ngo ambaye ametaka waandaaji wafanye mabadiliko.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni