Wananchi wa Kata ya Usagara, wilayani Misungwi wakimshangilia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga wakati alipokuwa akizungumza na wananchi hao katika Viwanja vya Gulio mjini Usagara. Wananchi hao walimwambia Waziri Kitwanga wanaikumbuka ahadi ya Rais John Magufuli wakati akiwa anamnadi Mbunge huyo kipindi cha kampeni, kuwa suala la maji atalishughulikia Rais mwenyewe. Hivyo wanamuomba Mbunge wao ashirikiane na Rais huyo ili maji yaweze kupatikana kwa haraka zaidi. Picha zote na Felix Mwagara.
Kikundi cha Burudani kinachoitwa Mawe Matatu cha Kata ya Usagara, wilayani Misungwi kikitoa burudani kabla ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kulia-aliyekaa) kuzungumza na wananchi wa kata hiyo katika Viwanja vya Gulio mjini Usagara. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga aliwashukuru wananchi hao kwa kumchagua na pia atahakikisha kero zote anazitatua. Hata hivyo, wananchi hao,walimwambia Waziri Kitwanga wanaikumbuka ahadi ya Rais John Magufuli wakati akiwa anamnadi Mbunge huyo kipindi cha kampeni, kuwa suala la maji atalishughulikia Rais mwenyewe. Hivyo wanamuomba Mbunge wao ashirikiane na Rais huyo ili maji yaweze kupatikana kwa haraka zaidi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni