.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 27 Januari 2016

MIKWAJU YA PENATI YAIBEBA LIVERPOOL KUTINGA FAINALI ZA CAPITAL ONE


Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema hakuangalia penati zilizoibeba Liverpool kutinga katika fainali za Kombe la Capital One na kuelekea katika nafasi ya kutwaa kombe lake la kwanza akiinoa timu hiyo msimu huu.

Katika mchezo huo Marko Arnautovic alifunga bao na kuifanya Stoke kulingana kwa magoli na Liverpool kwa manufaa ya goli la ugenini lakini machungu yaliwakuta Stoke wanaonolewa na Mark Hughes wakati wa kupigiana mikwaju ya penati. Matokeo ya mchezo huo Liverpool 6-5 Stoke.

Golikipa anayelaumiwa mno wa Liverpool, Simon Mignolet alikuwa ni shujaa wa Liverpool baada ya kuokoa kwa kupangu penati za Peter Crouch na Marc Muniesa, na kuikatia tiketi timu yake ya kukutana na Manchester City ama Everton kwenye dimba la Wembley February 28.
                           Joe Allen akimpoteza kipa wa Stoke na kupachika bao la penati 
                  Kipa wa Liverpool Simon Mignolet akipangua penati ya Peter Crouch

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni