Muigizaji filamu Muingereza Idris
Elba anatarajiwa kuwatahadharisha wabunge kuhusiana na kukosekana kwa
fursa kwa waigizaji wenye ngozi nyeusi kwenye Televisheni za
Uingereza.
Muigizaji huyo ambaye naye
alikumbana na hali hiyo, amesema alilazimika kwenda Marekani ili
kuweza kupata kufikiriwa kupewa nafasi ya kuwa muigizaji mkuu.
Elba ameongeza kuwa watu kwenye
ulimwengu wa televisheni si sawa na watu wengine waliokwenye
ulimwengu halisi, hivyo televisheni zipo katika hatari ya kutoonyesha
uhalisia wa jamii.
Elba mwenye miaka 43 atatoa kauli
hizo wakati akitoa hotuba ya uzoefu wake Jijini London huko
Westminster, na kuhudhuriwa na wabunge wapatao 100 na watendaji wakuu
wa Televisheni Uingereza.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni