.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 11 Januari 2016

NAIBU WAZIRI MASAUNI AWAONYA WANAOCHAFUA SERIKALI KUHUSIANA NA OPERESHENI KAMATA WAHAMIAJI HARAMU

Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ( pichani juu ) amewataka Maafisa Uhamiaji kutotumia nafasi ya kukamata wahamiaji haramu kinyume na matakwa ya Serikali pamoja na Sheria za nchi.

Hayo aliyazungumza katika Ofisi kuu ya Uhamijai Zanzibar iliyopo eneo la Kilimani alipofanya ziara yake ya kikazi ili kujionea shughuli za utendaji wa ofisi hiyo.

Waziri huyo amesema kuwa Serikali chini ya Idara ya Uhamiaji itapambana na wahamiaji waliopo nchini bila vibali ama kufuata kanuni na sheria zinazoruhusu ukaazi wao na si vinginevyo. Hivyo wageni wote wenye vibali vinavyowaruhusu kuwepo nchini hawato bugudhiwa kwa namna yoyote ile, na yeyoye atakae bainika kunyanyasa wageni hao wenye vibali atachukuliwa hatua za kinidhamu.

“Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine duniani kote tunapenda wageni, tunajua kwamba watalii, na wawekezaji waliopo nchini wana mchango mkubwa katika kuinua uchumi wa taifa letu, hivyo hatuwezi kuwafukuza ama kuwanyanyasa kama wako nchini kihalali” alisema Bw. Masauni.

Aidha amewataka maafisa wa uhamijia kuto tumia zoezi hilo la kubaini wakaazi haramu kwa manufaa yao na yeyote atakae bainika kutumia zoezi hilo kinyume na agizo la serikali atashughulikiwa kwani serikali haijapanga kuonea wala kunyanyasa mtu yeyote yule.

Naibu huyo aliongeza kuwa sheria zilizopo nchini ni kwa ajili ya manufaa ya nchi hivyo ni lazima kila mtu aziheshimu na kuwa Serikali haina lengo la kutumia sheria hizo kukandamiza wageni.

Pamoja na hayo Masauni alisema kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga kutatua kero za wananchi, hivyo Idara ya Uhamiji itaendelea kuwatumikia wananchi kwa weledi wa hali ya juu na kuhakikisha kero zote za awali zinatatuliwa. MWISHO.

(IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO MAMBO YA NDANI YA NCHI)



Hakuna maoni :

Chapisha Maoni