Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipata maelezo ya uboreshaji unaoendelea kufanyika wa kiwanja cha Ndege Terminal Two kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Eng. Suleiman Suleiman jijini Dar es Salaam.
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh.Prof. Makame Mbarawa ameagiza watumishi wa Tassisi zote zinazotoa huduma katika viwanja vya ndege hapa nchini kuwajibika kwa Mameneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) wanaosimamia viwanja ambavyo watumishi hao wamepangiwa kufanya kazi.
Mh. Mbarawa ametoa agizo hilo jana wakati alipofanya ziara ya siku moja kwenye Makao Makuu ya TAA ambapo pamoja na mambo mengine alikagua ujenzi unaondelea wa jengo la tatu la abiria (TBIII), na kituo cha Zimamoto na Uokoaji.
Pia alitembelea mradi wa usimikaji wa vivuko vipya vya abiria (Passenger Boarding Bridges) na usimikaji wa mitambo mipya ya kufua umeme wa dharura (Standby Generators) iliyopo katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Akizungumza na menejimenti ya TAA ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Suleiman S. Suleiman katika Ofisi za TAA ikiwa ni sehemu ya majumuisho ya ziara yake, Prof. Mbarawa aliwapongeza TAA kwa kazi nzuri wanayoifanya hususan katika uboreshaji wa muindombinu na kuhudumia wateja.

Hata hivyo alisema pamoja na sifa hiyo nzuri, kuna haja kwa TAA kuwa mdhibiti wa taasisi nyingine zote zinazofanyakazi katika viwanja vya ndege hapa nchini kama njia ya kuepuka kuchafua sifa nzuri ya viwanja hivyo na nchi kwa ujumla.
“ Pamoja na kazi nzuri mnayoifanya,nadhani wakati umefika sasa kwa taasisi zote zinazotoa huduma katika viwanja vya ndege hapa nchini ziwe chini ya TAA”, alisema Prof. Mbarawa huku akisisitiza umuhimu wa taasisi hizo kufanya kazi kwa kushirikiana kama timu moja.

“Nyinyi ndio kioo katika jamii yetu, taasisi nyingine mfano uhamiaji wakachelewa kugonga mhuri kwenye hati za kusafiria, watu hawatambui kama ndio wao waliochelewesha na lawama watawatupia nyinyi,” alisisitiza Mh. Mbarawa na kuongeza kwamba anafanya utaratibu wa kuwasiliana na Wizara zote zinazohusiana na taasisi hizo ili kupanga utaratibu muafaka.
Mbali na idara ya uhamiaji, taasisi nyingine zinazotoa huduma kwenye viwanja vya ndege ni pamoja na Idara ya maliasili, afya, kilimo, mifugo, madini, polisi na kitengo cha kuzuia madawa ya kulevya.
Mh. Mbarawa pia ameiagiza TAA kubuni mikakati ya kuongeza ukusanyaji wa mapato zaidi ili iweze kujiendesha na pia ihakikishe kuwa inaepukana na matumizi yasiyo ya lazima. Aliitaka watumishi wa TAA kuzingatia uadilifu na weledi katika utendaji wao wa kazi na kuhudumia wateja ikizingatiwa kuwa viwanja vya ndege ni kioo cha nchi.
“Nisingependa taarifa za matukio mbalimbali yanayotokea kwenye viwanja niyasikie au kuyaona kwenye vyombo vya habari wakati mimi mwenyewe sijui, hivyo tujenge utamaduni wa kuwa waadilifu na tufanye kazi kwa kuzingatia weledi, tuepukane na matukio ya hovyo,” alisisitiza Mh. Mbarawa.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi S.S.Suleiman alimhakikishia Waziri Mbarawa kutekeleza maagizo yake, likiwemo la kubuni mbinu mpya za mapato, na hata kuweka utaratibu wa kumpatia taarifa mbalimbali zinazotokea kwenye viwanja kabla hazijapelekwa sehemu nyingine yeyote, kwa ajili ya utekelezaji na kujenga uhusiano mzuri baina ya mamlaka na wizara kwa ujumla.
“Kuhusu mapato tunauhakika wakati wa jengo la tatu la abiria likifunguliwa yataongezeka, lakini tunaahidi kubuni mbinu nyingi zaidi, ili tuwe na vyanzo vya uhakika vya mapato,” alisema Mhandishi Suleiman. Alisema kukamilika kwa jengo hilo kutaongeza idadi ya abiria watakaosafiri na ndege za ukubwa mbalimbali ikiwemo 380 Airbus yenye uwezo wa kubeba abiria 300.
Awali Mh. Mbarawa alipotembelea ofisi za zimamoto zilizopo JNIA, alielezwa wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vifaa na hususan magari ya zimamoto ambayo mbali na kuhudumia viwanja vya ndege, wakati mwingine kulazimika pia kusaidia jamii endapo nyumba zao zinakumbwa na majanga ya moto.
Imetolewa na kitengo cha Habari na Mahusiano na Sheria TAA.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni