Manchester City imekwea kileleni mwa
Ligi Kuu ya Uingereza kwa muda baada ya kuichakaza Crystal Palace kwa mabao
4-0, kabla ya Leicester kurejea tena kileleni baadae.
Katika mchezo huo mshambuliaji
Sergio Aguero alipachika mabao mawili katika mchezo huo, ambao
ulishuhudia pia David Silva akitikisa nyavu, huku bao la kwanza
likipachikwa na Fabian Delph.
Sergio Aguero akiachia shuti lililoingia wavuni na kuandika bao lake la pili katika mchezo huo
Katika mechi nyingine John Terry
amefunga bao lililozua utata katika dakika ya 98, na kuipatia Chelsea
pointi moja baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Everton.
Everton walianza kuongoza baada ya
Terry kujifunga, na kisha Kevin Mirallas kufunga bao la pili, hata
hivyo Diego Costa na Cec Fabregas walisawazisha na kufanya matokeo
kuwa 2-2.
Ramiro Funes Mori aliongeza bao la
tatu kwa Everton katika dakika ya 90, kabla ya John Terry kusawazisha
kwa bao la kisigino ambalo inasadikiwa kuwa alikuwa ameotea kabla ya
kufunga.
John Terry akifurahia goli alilofunga na mashabiki wa Chelsea
Katika mechi zingine za Ligi Kuu ya
Uingereza matokeo yalikuwa Tottenham 4 - 1Sunderland, Bournemouth 3-
0 Norwich, Man City 4 – 0 Crystal Palace, Newcastle 2 - 1West Ham,
Southampton 3- 0 West Brom na Aston Villa1- 1 Leicester.




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni