.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 16 Januari 2016

UGAIDI TENA BURKINA FASO, SAFARI HII WATU 27 WAFARIKI DUNIA BAADA YA MAGAIDI KUITEKA HOTELI YA SPLENDID

Watu 27 wamefariki dunia katika shambulio la hoteli ya kitalii ya Splendid katika mji mkuu wa Burkina Faso , Ouagadougou. 

Taarifa zaidi zinasema kuwa watu wengine 126 wamefanikiwa kuokolewa na vikosi vya kijeshi vya nchi hiyo vikisaidiwa na wanajeshi wa Ufaransa baada ya kuizingira hoteli hiyo kwa muda baada ya kuvamiwa na kutekwa na wapiganaji wanne waliokuwa na silaha nzito. 

Kundi la Al-Qaeda la islamic Maghreb{AQIM} limedai kuhusika katika tukio hilo. 

Hoteli hiyo ilitekwa kwa muda wa saa 15 kabla ya vikosi vya kijeshi kuingilia kati na kufanikiwa kuwaokoa watu hao. Watu 23 wa mataifa 18 tofauti walifariki katika tukio hilo.
                               Wanajeshi wakiwa tayari kwa lolote walipoizingira hoteli hiyo

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni