Shirika la Afya Duniani (WHO)
limetahadharisha kuwa virusi vya Zika vinatarajiwa kusambaa karibu
katika mataifa yote ya Amerika.
Maambukizi ya virusi hivyo
vinavyosambazwa na mbu husababisha homa, maumivu ya misuli na kichwa,
na tayari umo katika mataifa 21 ya Caribbean, Kaksakzini na Kusini
mwa Amerika.
Virusi vya Zika vinahusishwa na
watoto wanaozaliwa na vichwa vidogo na kwenye baadhi ya mataifa
wanawake wanashindwa kutunga mimba. Hakuna dawa wala chanjo ya
ugonjwa huo.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni