.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 4 Februari 2016

FOS YATOA RIPOTI YA UTAFITI WA USHIRIKISHWAJI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI MKUU 2015 JIJINI DAR


(Picha na Fredy Njeje Blogs za Mikoa)

Kitengo cha Haki
za jinsia cha Oxfam nchini Tanzania Fahamu Ongea Sikilizwa(FOS) imezindua
kitabu chake cha utafiti kughusu taarifa za kushiriki kwa wanawake kati masuala
ya uchaguzi mkuu maka 2015 na 2016 nchini Tanzania.

Uzinduzi wa
taarifa hiyo umefanyika jana jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Double view na Meneja wa kitengo cha haki
za binadamu na jinsia kutoka Oxfam Bi. Rashida Shariff huku akieleza baadhi ya
mikoa iliyofanyiwa utafiti huo kuwaTanzania bara kwa mikoa nane ikiwemo
Shinyanga, Dodoma, Tanga, Arusha, Dar es
salaam, Morogoro,Lindi na Mwanza na Tanzania visiwani Zanzibar ni Kusini Unguja

Bi. Rashida
amebainisha lengo kuu la utafiti huo likiwa ni kuwapauwezo wa kujiamini wanawake
kushiriki kikamilifu katika kujitokez kikamilifu kupiga kura pamoja na kujikita
kwenye masuala ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi nchini bila woga.

Aidha
ameongeza kuwa utafiti umelenga kupata changamoto za wanawake walizokuwa
wanapata hususani kwa wagombea ambapo wagombea sita wanawake kutoka katika
vyamba mbalimbali vya siasa Mh. Angelina Mabula, Anna Mghwira, Nancy Mrikaria,
Khadija Msawira, Magreth Mshenene na Mh. Safia Mkamama wametumiwa kuelezea
changamoto zilizowakabili na mafanikio waliyoyapata ikiwemo ni pamoja na
kuongeza kujiamini
Kwa upande
wake aliyekuwa mgombea urais kwa kupitia Chama cha ACT -Wazalendo Anna Ngwila
amesema kuwa ushiriki wa wanawake katika uchaguzi bado umeelekezwa kwenye
ushabiki ambapo wanawake hutumiwa katika vyama kwa lengo la kutoa kura zao
kuliko wao wenyewe kugombea.

Bi Anna
akitolea mfano yeye mwenyewe alisema kuwa changamoto aliyokumbana nayo ni ndani
ya vyama ilikuwa ni kutiliwa mashaka kama ataweza mikikimikiki ya uchaguzi
lakini wanasahau kuwa wanawake nao wanaweza kutatua kero mbalimbali
zinazowakabili kijamii.

Naye mtafiti
mkuu wa utafiti huo Profesa Luth Meena ameongezea
kuwa taarifa hii itasaidia vyombo mbalimbali vya serikali ikiwemo vyama vya
siasa, msajili wa vyama vya siasa, tume za uchaguzi, vyombo vya habari,
TAKUKURU, pamioja na Asasi za kiraia na jamii kwa ujumla kuzumgumzia kwa
usahihi ikiwemo kuchukua hatua za kisera, kisheria katika kuleta usawa wa
kijinsia katika michakato ya uchaguzi huku ikiwapa uwezo wa kujiamini kwa
wanawake katika kushiriki katika masuala ya uchaguzi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni