Kinda Marcus Rashford ametikisa nyavu mara mbili na kutengeneza
bao la tatu wakati Manchester United ikiharibu mahesabu ya Arsenal ya
kuwania kutwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Old Trafford
Rashford ambaye alifunga mabao mawili katika mchezo wake wa kwanza na
timu ya wakubwa dhidi ya FC Midtjylland Alhamisi, alifunga bao la
kwanza katika dakika ya 28.
Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Danny Welbeck
alisawazisha bao na kuirejesha Arsenal katika mchezo, lakini Rashford
tena akinasa shuti lililopigwa na Herrera alipachika wavuni bao la
pili. Herrera alipachika bao la tatu na kisha Mesut Ozil kuifungia
Arsenal bao la pili na kufanya matokeo kuwa 3-2.
Kinda Marcus Rashford akipiga mpira wa kichwa uliojaa langoni mwa Arsenal
Danny Welbeck akifunga bao lake langoni mwa Manchester United
Nayo Tottenham imekwea pointi mbili nyuma ya vinara wa Ligi Kuu
ya Uingereza Leicester City baada ya kupigana kiume kutoka nyuma
baada ya kufungwa na kisha kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya
Swansea.
Mchezaji Alberto Paloschi aliwapatia wageni Swansea bao la
kuongoza, huku kabla ya Nacer Chadli kupadili mwelekeo wa shuti la
Kyle Walker. Bao la ushindi la Tottenham lilifungwa kwa shuti kali la
beki Danny Rose.
Beki wa Tottenham Danny Rose akishangilia bao lake lililoipaushindi timu yake
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)





Hakuna maoni :
Chapisha Maoni