.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 19 Februari 2016

KOCHA LOUIS VAN GAAL ASEMA KICHAPO WALICHOPATA KINAENDANA NA SHERIA YA MURPHY

Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal amesema kichapo alichopata cha mabao 2-1 kutoka kwa FC Midtjylland kinaendana na sheria ya Murphy, ambayo inasema kitu kisicho fanya vyema hakitofanya vyema.

Katika mchezo huo Memphis Depay aliipatia goli la kwanza Manchester United wakiwa ugenini katika mchezo wao wa awali wa Ligi ya Uropa hatua ya 32 bora, lakini Pione Sisto na Paul Onuachu waliwapatia wenyeji ushindi.

Kocha Van Gaal, ambaye kwa sasa hana wachezaji 13 kutokana na kuwa majeruhi, amempoteza pia kipa David de Gea wakati wa mazoezi ya kupasha joto mwili, hii sasa inamaanisha kitu kisicho fanya vyema hakitofanya vyema.
   Kipa Sergio Romero akipangua kimiujiza kwa mkono mmoja mpira wa kichwa na kuokoa goli 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni