.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 20 Februari 2016

KOCHA SUPER D AWAKILISHA RAMBIRAMBI ZA WADAU KWA FAMILIA YA MAREHEMU MOHAMED CHIBUMBUI

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimkabidhi mama mzazi wa marehemu Mohamed Chibumbui Hadija Likamba ubani uliotolewa na wadau mbalimbali wa mchezo wa masumbwi nchini kutoka Tanzania Boxing Fans pamoja na chama cha ngumi za ridhaa BFT katikati ni Baba mzazi Said Chibumbui Picha naSUPER D BOXING NEWS
  Rais waShilikisho la ngumi za Ridhaa Nchini BFT Mutta Rwakatare katikati akimkabidhi Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' mchango uliotolewa na wadau mbalimbali kwa ajili ya lambilambi ya marehemu Mohamed Chibumbui kilichotokea Mkoa wa Mtwara Wilaya ya Masasi kushoto ni katibu Mkuu wa shirikisho hilo Makole Mashaga Picha na SUPER D BOXING NEWS

                                                                                                 Na Mwandishi Wetu

KOCHA wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amekabidhi fedha za lambilambi kwa wafiwa wa bondiaMohamed Chibumbui ambaye alikuwa anachezea timu ya taifa ya mchezo wa masumbwi nchini

Chibumbui aliefaliki feb 10 alikuwa anasumbuliwa na ugojwa wa kisukari na alizikwa feb 13 katika kijiji cha Mihima kata ya Namupa Tarafa ya Mtama wilaya ya Lindi Mkoa wa Lindi

Bondia Mohamed Chibumbui aliezaliwa April 24 mwaka 1988

Alianza kujifundisha mchezo wa masumbwi mwaka 2003 akiwa chini ya kocha Juma Urungu 'Mkebezi' na timu ya mavituzi.

Baada ya hapo aliamia timu ya polisi kisha timu ya JKT na mwisho mapaka kifo kinamkuta alikuwa akichezea timu ya Magereza

Akizngumza wakati wa kupokea ubani uho uliotolewa na wadau mbalimbali wa masumbwi wakiongozwa na Rais wa Shilikisho la ngumi za Ridhaa Nchini BFT na Tanzania Boxing Fans 'TBF' inayowakutanisha wadau mbalimbali kwa njia ya mtandao wa Watsap Group mama wa marehemu.

Hadija Likamba ameshukuru kwa kufikiwa na lambilambi hiyo kutoka kwa wadau wa mchezo wa ngumi nchini na kuzidi kuwaombea duwa ili mchezo wa ngumi usonge mbele.

Nae baba wa marehemu Said Chibumbui amewashukuru wadau wote na kwamba wataendelea kushirikiana bega kwa bega ambapo watakaa kikao kwa ajili ya alobaini ya marehemu na kufikishiwa taarifa.

Marehemu alimuowa Ratifa Adrea june 7 mwaka 2008 na kubahatika kupata watoto wawili mmoja ni Alhaj Mohamed Chibumbui (7) na Abubakari Mohamed Chibumbui (2) jumla marehemu ameacha watoto wawili na mke mmoja.

Aliongeza kwa kusema kuwa shughuli nzima ya alobaini itafanyika nyumbani alipozaliwa marehemu tndika azimio tambukareli eneo la maputo

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni